Iain Gray ameiambia televisheni ya Press TV kuwa, chama chake kinapigania kujitenga Scotland na Ufalme wa Uingereza.Mkuu huyo wa chama cha Leba amesema kuwa, wakati umefika kwa Scotland kuamua kuhusu kujitenga na Ufalme wa Uingereza akisisitiza kuwa, nchi hiyo ina watu, utajiri na ukubwa wa kutosha wa kuwa nchi huru nje na Ufalme wa Uingereza.Siku ya Alkhamisi pia, Iain Gray aliikosoa vikali serikali ya Uingereza kwa kusababisha ukosefu mkubwa wa kazi miongoni mwa vijana wa nchi hiyo akisema kuwa haoni sababu kwa nini Scotland iendelee kuwa chini ya Ufalme wa Uingereza.
19 Machi 2011 - 20:30
Msimbo wa Habari: 275377
Abna inatuarifu kuwa:Kiongozi wa chama cha Leba cha Scotland amesema kuwa umefika muda wa nchi hiyo kujitenga na Ufalme wa Uingereza.